Marekani yashutumu hatua ya kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amelaani hatua ya Uingereza, Norway, Australia, Canada na New Zealand kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali kutokana na mzozo wa Gaza.

Marco Rubio alilaani hatua hiyo, akiandika kwenye mtandao wa X: alisema “Vikwazo hivi haviendelezi juhudi zinazoongozwa na Marekani kufikia usitishaji vita, kuwarudisha mateka wote nyumbani, na kumaliza vita”.

Aliyataka mataifa kubatilisha vikwazo hivyo, akiongeza kuwa Marekani “imesimama bega kwa bega na Israel.”

Uingereza imewawekea vikwazo Waziri wa Fedha Smotrich na Waziri wa Usalama wa Kitaifa Ben-Gvir kwa sababu ya “kuchochea ghasia za itikadi kali na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu za Wapalestina”.

Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich wote watapigwa marufuku kuingia Uingereza na mali yoyote nchini Uingereza itazuiwa kama sehemu ya hatua zilizotangazwa na waziri wa mambo ya nje.

Ni sehemu ya hatua ya pamoja na Australia, Norway, Canada na New Zealand iliyotangazwa Jumanne.

Ikijibu, Israel ilisema: “Inasikitisha kwamba wawakilishi waliochaguliwa na wanachama wa serikali wanachukuliwa hatua za aina hii.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment