Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maelfu ya watu nchini Austria wamefanya mkesha wa kuwasha mishumaa kwa waathiriwa wa shambulio la ufyatuaji wa risasi shuleni ambapo watu 10 waliuawa.
Polisi walisema mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni mwanafunzi wa zamani, alijitoa uhai katika bafu la shule muda mfupi baada ya kutekeleza shambulizi hilo huko Graz siku ya Jumanne – likiwa ni baya zaidi katika historia ya hivi majuzi ya nchi.
Kisa hicho kilitokea katika shule ya upili ya Dreierschützengasse kaskazini magharibi mwa jiji.
Watu wengine 12 walijeruhiwa, wengine vibaya, na nia ya mshambuliaji huyo bado inachunguzwa, maafisa walisema.
Wanawake sita na wanaume watatu waliuawa katika shambulio hilo, na mwanamke wa nne alifariki baadaye hospitalini.
Shirika la habari la APA la Austria limeripoti kuwa saba kati ya waliouawa walikuwa wanafunzi.
Astrid, mwanamke anayeishi na mumewe Franz katika orofa ya chini ya jengo la makazi karibu na shule hiyo, aliambia BBC kwamba alikuwa amemaliza tu kufua aliposikia milio ya risasi.
Alisema: “Nilisikia milio ya risasi. Nyingi, moja baada ya nyingine. ‘Poof… poof… poof…. poof…’ tena na tena. Niliingia aliko mume wangu na nikamwambia: ‘Kuna mtu anapiga risasi!’
Kufikia Jumanne alasiri, foleni ndefu zilikuwa zinashuhudiwa nje ya kituo cha uchangiaji damu huko Graz.
“Leo ni siku ngumu kwetu sote Graz. Niko hapa [kuchangia] damu yangu kusaidia watu wengine wanaohitaji,” Stephanie Koenig mwenye umri wa miaka 25 aliambia shirika la habari la Reuters.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.