Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Elon Musk asema ‘anajutia’ baadhi ya ujumbe aliyochapisha kuhusu Donald Trump
Elon Musk ameomba radhi katika mtandao wa X akielezea masikitiko yake juu ya vita vyake vya maneno na Rais Donald Trump wiki iliyopita, na kukiri kwamba “baadhi” ya ujumbe wake wa kumshambulia kiongozi huyo wa taifa “ulivuka mpaka.”
“Najutia baadhi ya ujumbe wangu kuhusu Rais Donald Trump wiki iliyopita. Ulivuka mpaka,” tajiri huyo aliandika kwenye mtandao wa kijamii anaoumiliki mapema Jumatano asubuhi.
Wawili hao walijikuta katika mzozo hadharani, baada ya mmiliki wa Tesla kupinga mswada wa ushuru wa Trump.
Ujumbe wake unawadia baada ya Trump kutangaza kuwa uhusiano wao umefikia kikomo na kwamba hana nia ya kuurekebisha.
Bajeti hiyo, ambayo inajumuisha punguzo kubwa la ushuru na matumizi zaidi ya ulinzi, ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi mwezi uliopita na sasa ipo katika Bunge la Seneti.
Musk aliwataka Wamarekani kutoa wito kwa wawakilishi wao “kutoupitisha muswada huo” kwa sababu anaamini “utasababisha mdororo wa uchumi katika nusu ya pili ya mwaka”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.