Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ii. Utahisi kila wakati una mambo mengi yasiyoisha
iii. Utakosa hamasa ya kufanya mambo muhimu
iv. Utakosa ari ya kufanya mambo kwa haraka
v. Utakuwa ni mtu usiye na vipaumbele maishani
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Ya Udhaifu
– Utakuwa ni mtu usiye na vipaumbele maishaniUdhaifu wa tano ambao utakutana nao unapokuwa mtu wa kughairisha mambo kwenye maisha yako, utakuwa ni mtu usiye na vipaumbele kabisa.
Kitu kimojawapo muhimu sana katika maisha yako ni uwezo wa wewe kuamua, ni jambo gani muhimu la kufanywa sasa hivi na jambo ambalo sio muhimu linaloweza kusubiri.
Ukikosa uwezo huu, itakusababishia uwe ni mtu ambaye kila wakati unatumia nguvu, muda na pesa zako kufanya mambo ambayo hayana mchango mkubwa kwenye maisha yako na utajiona kama hupati matokeo unayoyatafuta.
Watu ambao wanatawaliwa na mfumo wa Limbic ni watu ambao huwa wanashindwa kuweka vipaumbele vya kufanya mambo muhimu kabla ya kujikita katika mambo yasiyo ya umuhimu kwenye maisha yao.
Kama tulivyoona hapo awali kuwa mfumo wa limbic ukikutawala, kitu kimoja kimoja kinachotokea ni kuwa utapenda vitu vya kujiburudisha zaidi kuliko vile ambavyo vinakujenga kwa sababu wenyewe una sehemu ya kupenda kujiburudika (pleasure centre).
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.