Jeshi la wanamaji la Israel lashambulia mji wa bandari wa Hudaydah unaodhibitiwa na Wahouthi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,Picha ya setilaiti ya bandari ya Hudaydah

Meli za jeshi la wanamaji la Israel zimeshambulia maeneo ya bandari ya Hudaydah nchini Yemen inayodhibitiwa na Wahouthi.

Jeshi la Israel limesema katika taarifa kwamba mashambulizi hayo yalifanywa kujibu makombora ya Wahouthi yaliyoilenga Israel na yalilenga kusitisha matumizi ya bandari hiyo kwa “malengo ya kijeshi”.

Hakukuwa na ripoti za mara moja za majeruhi.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha moshi mweusi ukipanda kutoka bandarini, huku Televisheni ya al-Masirah inayoongozwa na Wahouthi ikiripoti mahsmabulizi mawili tofauti tofauti.

Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakirusha makombora mara kwa mara huko Israel wakishirikiana na Wapalestina huko Gaza. Siku ya Alhamisi, kombora la Wahouthi liliangushwa juu ya Jerusalem, huku mwezi uliopita moja liliupiga uwanja wa ndege mkuu wa Israel.

Mashambulizi ya Hudaydah, ambayo kwa njia isiyo ya kawaida yalitekelezwa na meli za jeshi la wanamaji badala ya ndege, yalifanywa alfajiri ya Jumanne asubuhi.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) awali lilitoa onyo la kuhama kwa wale wote waliokuwepo katika bandari ya Hudaydah, pamoja na bandari nyingine zinazodhibitiwa na Wahouthi za Ras Isa na Salif.

“Kutokana na utawala wa kigaidi wa Houthi kutumia bandari kwa shughuli zake za kigaidi, tunawaomba wote waliopo kwenye bandari hizi kuhama na kukaa mbali nazo kwa usalama wenu hadi taarifa nyingine,” msemaji wa IDF wa lugha ya Kiarabu Avichay Adraee aliandika kwenye X.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment