Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ii. Matumizi ya Pesa Zako
Katika Makala Hii Tutazungumzia Eneo la Kwanza
– Matumizi ya Muda
Matumizi ya muda wako ndio ishara ya kwanza unayohitaji kuichunguza ili kujua kama utafanikiwa ama la.
Kama wewe ni mtu ambaye kila wakati unatumia muda wako kwa mambo ambayo hayana faida kabisa kwenye maisha yako, na kisha unakosa muda kabisa wa kufanya mambo yenye faida, basi ujue hakuna namna utaweza kufikia malengo ambayo umejiwekea.
Hebu fanya zoezi dogo sana na ukague jinsi ambavyo ulitumia muda wako kwa siku ya jana.
Jaribu kufikiria tangu asubuhi hadi ulipoenda kulala usiku ulitumiaje muda wako?
Hebu jaribu kujiuliza ulitumia saa ngapi kufanya mambo yanayojenga?
Na ulitumia saa ngapi kufanya mambo yasiyojenga?
Hebu jaribu pia kufikiria kuhusu siku ya leo, hadi sasa umetumiaje muda wako?
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.