Ureno yailaza Uhispania katika Ligi ya Maitafa Ulaya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Ureno iliwashinda majirani zao Uhispania kwa mikwaju ya penalti na kuibuka washindi katika fainali mjini Munich na kushinda taji lao la pili la Ligi ya Maitafa Ulaya.

Cristiano Ronaldo aliisawazishia Ureno kwa mabao 2-2 katika dakika ya 61, lakini hakukuwa na cha ziada wakati mwamuzi alipoashiria kumalizika kwa muda wa kawaida.

Akitolewa nje kabla ya muda wa ziada, nahodha wa Ureno Ronaldo alishuka uwanjani na kulia machozi ya furaha baada ya Ruben Neves kufunga penalti ya ushindi kufuatia Diogo Costa kuokoa mkwaju wa penalti wa Alvaro Morata.

Washindi wa 2023, Uhispania walikuwa wameanza kufunga dakika ya 21 wakati Martin Zubimendi alipofunga bao la kwanza baada ya Ureno kushindwa kufurukuta.

Hata hivyo uongozi wao ulidumu kwa muda mfupi huku Nuno Mendes akipiga shuti la chini chini na kumpita Unai Simon na kuingia kwenye kona ya mbali ya wavu dakika tano baadaye.

Mikel Oyarzabal, ambaye alifunga bao la ushindi dakika za lala salama katika fainali ya Ubingwa wa Ulaya msimu uliopita dhidi ya England, aliirejesha La Roja kwenye nafasi yake kabla ya kipindi cha mapumziko.

Lakini Ronaldo aliokoa Ureno alipomrukia Marc Cucurella na kufikia krosi iliyopanguliwa na Mendes na kuunganisha mpira wavuni kutoka eneo la karibu.

Goncalo Ramos, Vitinha, Bruno Fernandes na Nuno Mendes wote walipiga penalti zao kwa utulivu kabla ya juhudi za Morata kuzimwa na Costa.

Na Neves alipofunga mkwaju wa mwisho, Ureno ikawa timu ya kwanza kushinda mataji mawili ya Ligi ya Mataifa – na kuwanyima Uhispania, ambao walikuwa wakigombea fursa sawa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment