HAWATAKUSHUKURU

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zipo nyakati ambazo “HAWATAKUSHUKURU” kama unavyoona unastahili…

Inawezekana kabisa ukawa unajitoa sana kwa ajili ya ndugu zako.

Unajinyima mambo mengi ili wao wasome.

Wapate chakula au watibiwe.

Ila cha kushangaza siku ukishindwa kufanya watakulaumu.

Tena kama vile haujawahi kuwasaidia.

Au haujawahi kusikia yule mtu ambaye hadi anaenda kukopa pesa za riba ili asaidie wazazi wake.

Matokeo yake, hao hao wazazi wanageuka na kuanza kumsema kuwa amewasahau.

Hii huwa inatokea hadi kwa wapenzi.

Mmoja wao anaweza kujitoa sana kwa ajili mwingine.

Yaani akajinyima mambo mengi binafsi.

Au hata kuwanyima ndugu zake.

Ila mwisho wa siku anapewa maneno kuwa yeye ni mbinafsi.

Mambo haya yanaumiza na yanakatisha tamaa.

Jambo la muhimu ni kukumbuka kuwa, sio binadamu wote huwa wana moyo wa SHUKRANI.

Wengi huwa ni walalamishi.

Wewe fanya kwa sehemu yako.

Na wale wasiotambua mchango wako leo watakuja kuelewa baadaye.

Kikubwa, usifanye sana kwao kwa kujiumiza kulikopitiliza…

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment