Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Viongozi watano wa kundi la mrengo wa kulia la Proud Boys, ambao walipatikana na hatia ya kuhusika na ghasia zilizotokea Bungeni za Januari 6, 2021, wameishtaki serikali ya Marekani wakitaka dola milioni 100 (£74m), kwa madai kuwa haki zao zilikiukwa wakati waliposhtakiwa.
Watano hao walipatikana na hatia ya kupanga njama na kushiriki katika ghasia za kutaka kubadilisha matokeo baada ya Rais Donald Trump kushindwa katika kinyang’anyiro cha mwaka 2020.
Kuna wale ambao Trump aliwasamehe ama kubatilisha adhabu zao mapema mwaka huu.
Kesi hiyo, iliyowasilishwa Florida siku ya Ijumaa, inadai kuwa maafisa wa FBI na waendesha mashtaka walikuwa na upendeleo wakati wa kuendesha kesi zao.
Wanahoji kuwa haki zao za kikatiba zilikiukwa kwa “kuwaadhibu na kuwakandamiza washirika wa kisiasa” wa Trump.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.