Jeshi la Mali latangaza kuzima shambulio la wanamgambo mjini Tumbuktu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Mali

Jeshi la Mali linasema kuwa limetibua “jaribio la wapiganaji wa kigaidi kuvamia” kambi ya kijeshi ya Timbuktu kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakazi wa jiji hilo la kihistoria walielezea kusikia milio ya risasi na makombora, wakisema kuwa wanamgambo walilenga maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.

Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa X, jeshi la Mali lilisema siku ya Jumatatu kuwa hali imedhibitiwa na kwamba wanajihadi 13 wamezuiliwa na silaha, magari na vitu mbalimbali kupatikana.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa msako unaendelea kufanywa kote Timbuktu. Lakini haikutaja kundi lililohusika na shambulio hilo.

NIM, kundi la Al-Qaeda linalounga mkono wanamgambo hao wa kijihadi, hapo awali lilidai kufanya mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na shambulio la Jumapili, lililolenga kambi ya kijeshi ya Boulkessi katikati mwa Mali, wakidai udhibiti wa kambi hiyo.

Zaidi ya wanajeshi 30 waliuawa katika shambulio la Jumapili, kwa mujibu wa vyanzo vilivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters, hata hivyo idadi hiyo haijathibitishwa na mamlaka.

Lakini, jeshi la Mali bado halijafichua idadi yoyote rasmi ya maafisa wake walioathiriwa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment