Uingereza yatishia kumshitaki Abramovich – Kunani?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

,

Serikali ya Uingereza imetishia kumshtaki mmiliki wa zamani wa Klabu ya Soka ya Chelsea Roman Abramovich ili kushinikiza fedha zitakazotokana na mauzo ya klabu hiyo zinawafaidi raia wa Ukraine.

Mapato ya takriban pauni bilioni 2.5 yamezuiliwa katika akaunti ya benki ya Uingereza tangu kuuzwa kwa klabu hiyo, baada ya Bw Abramovich kuwekewa vikwazo kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022.

Serikali ya Uingereza inataka pesa hizo zitolewa kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Ukraine, lakini Bw Abramovich anataka ziende kwa “waathiriwa wote wa vita nchini Ukraine”.

Katika taarifa ya pamoja, Kansela Rachel Reeves na Waziri wa Mambo ya Nje David Lammy walisema: “Mlango wa mazungumzo utaendelea kuwa wazi, tuko tayari kufuatilia hili kupitia mfumo wa mahakama tukuhitajika kufanya hivyo.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment