Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Huu ni kwaajili yako kama hadi watu wako wa karibu wamekukatia tamaa…
Kuna watu wengi sana ambao wameshakukatia tamaa…
…Wanaamini hauwezi tena kuwa vile UNAVYOSEMA utakuwa.
Wengine wanaona UMRI wako umeshaenda sana na UMESHACHELEWA.
Kuna ambao wanaona kwa MAKOSA uliyofanya hakuna namna unaweza KUREKEBISHA na kuinuka tena.
Si unawafahamu wale ambao wanaona HAUSTAHILI kwa sababu ya UDHAIFU wako wanaoujua.
Kiufupi ni kuwa, kila siku utakutana na watu ambao HAWAAMINI Kama unaweza KUFANIKIWA ZAIDI ya LEO.
Kama leo unapitia hali hii, napenda kukumbusha kuwa “WEWE USIJIKATAE, JIKUBALI”
Hata Kama wao wamekukataa wewe amua KUJIKUBALI, amua kuendelea KUPAMBANIA unachokiamini…
…na kuna siku MATOKEO utakayoyapata yatakuwa ni SOMO kwao kuwa MUNGU anaweza KUWAWEZESHA na KUWAINUA wale waliokataliwa na wengine.
Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu comment neno “SITAJIKATAA, Mimi Nina Jikubali”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.