Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watafiti wa wanyamapori wamenasa na kuchapisha picha ya mmoja wa wanyama wa Kiafrika walio hatarini kutoweka, swala adimu na asiyejulikana kwa kiasi fulani anayeitwa Upemba Lechwe.
Watafiti walifanya uchunguzi eneo la kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambao waliwaona swala 10 tu, ikionesha idadi yao iko chini ya 100.
Manuel Weber, ambaye aliongoza utafiti, alielezea spishi kama “ukingoni kutoweka”, kulingana na taarifa kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Upemba.
Upemba Lechwe wanajulikana kwa kukosa mistari meusi kwenye miguu yao tofauti na swala wengine katika eneo hilo, watafiti wanasema.
Hata hivyo alionya kuwa ni mazingira “ya changamoto kubwa” kuhusiana na uhifadhi. Alisema masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu, uvuvi na uwindaji yanaweka maeneo ya ikolojia “hatarini”.
Kulingana na utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la African Journal of Ecology, hili lilikuwa jaribio la kwanza la kuchunguza viumbe hao katika zaidi ya miaka 50. DR Congo ina historia ya picha za wanyamapori maarufu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.