Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maelfu wanamkumbuka George Floyd katika kumbukumbu ya miaka mitano tangu alipofariki dunia aliyeuawa na polisi.
Mauaji ya Floyd, mwanamume mweusi huko Minneapolis yalisababisha maandamano nchini Marekani kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi.
Siku ya Jumapili, familia ya Floyd ilikusanyika katika mji wao wa Houston karibu na kaburi la Floyd kwa ibada iliyoongozwa na Kasisi Al Sharpton, huku Minneapolis.
Hata hivyo, kile ambacho wengi walikisifu kama “juhudi” ya kitaifa kukabiliana na ubaguzi wa rangi baada ya kifo cha Floyd, inaonekana kufifia wakati wa utawala wa Rais Donald Trump kwa kurudisha nyuma mageuzi ya polisi huko Minneapolis na miji mingine.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.