Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Takribani Wapelestina 54 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya anga ya Israeli usiku wa kuamkia leo, ikiwa ni pamoja na shambulizi dhidi ya shule ambayo inahifadhi wakimbizi katikati mwa Gaza, wakurugenzi wawili wa hospitali wameiambia BBC.
Shule ya Fahmi Al-Jargwi iliyopo mjini Gaza imekuwa na makazi ya mamia ya familia zilizofurushwa kutoka mji wa Beit Lahia, kwa sasa inakabiliwa na mashambulizi makali ya Israeli.
Msemaji wa Kikosi cha Ulinzi wa Raia wa Gaza kinachoendeshwa na Hamas alisema miili 20, ikiwa ni pamoja na ya watoto, ilipatikana – mingi ilichomwa vibaya, baada ya moto kuteketeza madarasa mawili yaliyogeuzwa kuwa makazi.
Jeshi la Israel (IDF) lilisema lililenga “kituo na udhibiti wa Hamas na Islamic Jihad”.
IDF ilisema eneo hilo lilikuwa linatumiwa “na magaidi kupanga… mashambulizi dhidi ya raia wa Israel na wanajeshi wa IDF”, na kuishuutumu Hamas kwa kutumia “wakazi wa Gaza kama ngao”.
Moto ulikuwa kila mahali. Niliona miili iliyoungua ikiwa imelala chini,” Rami Rafiq, mkazi anayeishi karibu na shule hiyo, alisema katika mahojiano na BBC kwa njia ya simu. “Mwanangu alizimia alipoona tukio hilo la kutisha.”
Kanda za video zilizosambazwa mtandaoni zilionyesha moto mkubwa ukiteketeza sehemu za shule, zikiwa na picha za waathiriwa walioungua vibaya, wakiwemo watoto, na walionusurika wakiuguza majeraha mabaya.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.