Uganda yasitisha ushirikiano wake wa kiulinzi na Ujerumani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Uganda Jumapili ya wiki hii lilitangaza kusitisha ushirikiano wote wa kiulinzi na Ujerumani, ikimtuhumu balozi wa Berlin, Matthias Schauer kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi huyo.

Wanajeshi wa Uganda (UPDF) wakiwa katika Mji wa Bunagana, DRC, Machi 2023.
Wanajeshi wa Uganda (UPDF) wakiwa katika Mji wa Bunagana, DRC, Machi 2023. AFP – GLODY MURHABAZI

Msemaji wajeshi la UPDF Chris Magezi, katika taarifa amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ripoti za kuaminika za kiintelejensia kuwa balozi huyo anajihusisha na vitendo vinavyotishia usalama wa kitaifa.

Licha ya kwamba taarifa hiyo haikuweka wazi vitendo hivyo vinahusisha nini hasa, taarifa hiyo imemtuhumu balozi huyo kwa kushirikiana na makundi ya kisiasa na kijeshi yanayopinga serikali ya Uganda.

Muhoozi kainerugaba - Mkuu wa majeshi nchini Uganda
Muhoozi kainerugaba – Mkuu wa majeshi nchini Uganda REUTERS – Abubaker Lubowa

Tangazo hilo la jeshi ambalo linazidisha mvutano kati ya Uganda na Ujerumani, inafuatia tangazo lingine la serikali ijumaa iliopita ambayo ilionya kuwa baadhi ya balozi za ulaya zinaunga mkono makundi ya uasi na wasaliti, ujumbe huo ulionekna kumlenga balozi Schauer.

Schauer ambaye amehudumu kama balozi wa Ujerumani nchini Uganda tangu 2020 amekabiliwa na  ukosoaji baada ya mkutano wake wa faragha  na kaka yake rais Yoweri Museveni ambapo anadaiwa kukosoa tabia ya mtoto wa Museveni na mkuu wa majeshi Muhoozi kainerugaba kwenye mitandao ya kijamii.

Bado haijafahamika namna hatua hiyo itaathiri uhusiano mpana wa kijeshi kati ya Uganda na Ujerumani, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa msaada wa vifaa na kiufundi kwa jeshi la Uganda.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment