Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hakuna msisimko wowote hata wakati unapozungumza na raia. Watoto wanapata shida kutazama. Ni nini kinachoweza kumshangaza mtoto anayeishi kati ya wafu, wanaokufa, wanaongojea kufa? Huku njaa ikiwamaliza.
Wanasubiri kwenye foleni ama kupata mgao mdogo au wakose kabisa.
Wamemzoea mpigapicha anayefanyakazi kwa ajili ya BBC.
Anashuhudia njaa wanayopitia, kufa kwao, na kufunikwa taratibu kwa miili yao – au vipande vya miili yao – katika sanda nyeupe ambazo zinaandikwa majina yao, kama yanajulikana.
Kwa miezi 19 ya vita, na sasa chini ya mashambulizi mapya ya Israel, mpigapicha huyu wa eneo – ambaye jina lake tumelificha kwa sababu ya usalama wake – amesikiliza kilio cha uchungu cha manusura katika ua wa hospitali.
Alimtafuta Siwar Ashour, msichana wa miezi mitano ambaye sura yake imedhoofika na kilio cha uchovu katika hospitali ya Nasser huko Khan Younis kimekuathiri sana.
Alikuwa na uzani wa zaidi kidogo tu ya kilo 2. Mtoto wa kike wa miezi mitano anayepaswa kuwa na kilo 6 au zaidi.
Siwar ameruhusiwa kurejea nyumbani.

Siwar ni mtulivu, anajihisi salama na uwepo wa wanawake wawili. Hawezi kunyonya maziwa ya kawaida kwa sababu ya tatizo la mzio. Chini ya hali ya vita na zuio la Israeli kwa misaada inayowasili, kuna uhaba mkubwa wa maziwa.
Najwa, mamake Siwar, 23, anaeleza kuwa hali ya mtoto wake iliimarika kidogo alipokuwa hospitalini, lakini sasa imeanza tena kuzorota kwa sababu ya ukosefu wa maziwa.
Nzi hujaa mbele ya uso wa Siwar. “Hali ni mbaya sana,” anasema Najwa, “wadudu wanamjia, lazima nimfunike na kitambaa ili wasimguse”.
Siwar ameishi na sauti ya vita tangu Novemba mwaka jana alipozaliwa. Milio ya risasi na ndege zisizo na rubani za Israel zinazunguka juu ya anga. Sauti ya vifaru, ndege za kivita, na roketi ni kubwa sana na ziko karibu nasi. Siwar anaposikia sauti hizi, anashtuka na kuanza kulia.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.