Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Watu Wanaokuamini (Those Who Believe In You)
ii. Watu Watakaokutambulisha (Those Who Will Introduce You).
iii. Watu Watakaokutoa Nje Ya Faraja Yako (Those Who Will Take You Out Of Your Comfort Zone).
iv. Watu Watakaokusaidia (Supporters)
v. Watakaokusaidia Kiroho (Spiritual Coverage)
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina Ya pili
– Watu Watakaokusaidia (Supporters)
Kwenye kila hatua ya maisha yako kuelekea maono yako, Mungu ameandaa watu mbalimbali wa kukutambulisha na kukuunganisha kwa watu wenye fursa unazozihitaji (Destiny Connectors).
Kwenye kila hatua mpya unahitaji utambulisho mpya. Kuna watu kinachowakwamisha ni kwa sababu haujapata mtu wa kukutambulisha mahali unapotakiwa kufika.
Kumbuka, kuna mahali jina lako linatakiwa kutajwa ambapo wewe hauna nafasi au uwezo wa kujitaja, unahitaji watu wa namna hii.
Ili Yusufu atimize maono yake ya muda mrefu ya kuwa kiongozi wa juu sana wa kitaifa, ilibidi atajwe na rafiki yake ambaye walikutana wote wakiwa wafungwa (Mwanzo 41 : 9 – 15).
Kuna watu ambao Mungu anakukutanisha nao leo ili kesho watumike kukutaja mahali fulani.
Hii ndio maana lazima ujifunze kumheshimu kila mtu kwani kuna wengine leo wanaonekana hawana faida kwako ila kesho watakuwa na faida kubwa sana kwenye maono yako.
Baada ya watu wengi kutokumwamini Sauli / Paulo na wengine kumkataa, ilibidi Barnaba atumie nafasi yake kumtambulisha ili aweze kukubalika (Matendo 9 : 26 – 27).
Kuna mahali watu hawatakukubali au kukupokea hadi upate mtu wa namna hii.
Kabla Yesu hajaanza huduma yake, ilibidi Yohana Mbatizaji amtambulishe kwa watu (Mathayo 3).
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.