Amini Tuu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hili ni maalumu kwa wote ambao waliahidiwa kitu na Mungu…

“Lakini AKIIONA AHADI ya Mungu HAKUSITA kwa KUTOAMINI, bali ALITIWA NGUVU kwa IMANI, AKIMTUKUZA Mungu;” Warumi 4:20

Kuna AHADI ambayo MUNGU huwa anampa mtu BINAFSI ambayo…

…wengine HAWAIJUI au wanaweza WASIIAMINI.

Unaweza kupita kwenye MAZINGIRA na HALI ambayo…

…ukijikagua inaonekana AHADI ya MUNGU juu ya UKUU wako haifanani na hali yako ya sasa.

Hii iliwahi kumtokea ABRAHAM.

Aliahidiwa kuwa baba wa mataifa…

…ila kwa miaka 25 akawa bado HAJAPATA MTOTO na UZEE UMESHAINGIA.

Alifanyaje?

Aliamua KUENDELEA kuweka MACHO yake kwenye kile MUNGU ALICHOSEMA (Akiiona).

Yeye alikuwa ANAIONA, inawezekana wengine walikuwa HAWAIONI.

Usiache KUAMINI kwa sababu wengine HAWAONI UNACHOKIONA.

Aliendelea KUMTUKUZA MUNGU.

Yaani, pamoja na kuwa MUDA ulikuwa UNAENDA na DALILI HAZIONEKANI…

…ila yeye aliendelea KUMSIFU MUNGU kwa kile ambacho alimuahidi akiamini kuwa ATAFANYA.

Leo, badilisha LUGHA YAKO.

Badala ya kusema “Mungu mbona UNACHELEWA Kufanya?”…

…anza kuwa kama ABRAHAMU,

Sema “MUNGU NAKUTUKUZA kwa sababu najua kile ULICHONIAHIDI UTAFANYA bila kujali HALI YANGU”.

USISITE KWA KUTOKUAMINI, ALICHOSEMA ATAFANYA.

Nakutakia Siku Ya Ushindi.

Kama umejifunza kitu…

Comment maneno…

“MUNGU NAKUTUKUZA kwa sababu najua kile ULICHONIAHIDI UTAFANYA bila kujali HALI YANGU”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment