Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali Uingereza itaanzisha matumizi ya dawa kemikali ya kuzuia hamu ya ngono kwa wenye makosa ya kingono, kama sehemu ya hatua za kupunguza hatari ya kurudia tena kufanya makosa hayo tena na kupunguza shinikizo kwenye mfumo wa magereza, ambao unaishiwa na nafasi.
Katika taarifa kwa Bunge Alhamisi kufuatia kutolewa kwa mapitio huru ya hukumu, Waziri wa sheria wa Uingereza Shabana Mahmood alisema kile kinachojulikana kama kuhasiwa kwa kemikali kitatumika katika magereza 20 katika mikoa miwili na kwamba anafikiria kuifanya kuwa kitendo cha lazima.
“Kwa kweli, ni muhimu kwamba mbinu hii ichukuliwe sambamba na mbinu za kisaikolojia ambazo zinalenga sababu nyingine za kuudhi, kama vilekuzuwia na udhibiti [wa ngongo],” alisema.
Ingawa hakiki ilionyesha matibabu hayatakuwa muhimu kwa baadhi ya wenye makosa ya kingono kama vile wabakaji wanaofanya vitendo hivyo kwa lengo la mamlaka na udhibiti, badala ya ngono kama tendo la kujifurahisha , Mahmood alisema tafiti zinaonyesha kuwa kuhasiwa kwa kemikali kunaweza kusababisha kupunguza uwezekano wa mtu kurudia kosa hilo kwa 60%
Kuhasiwa kwa lengo la kudhibiti uhalifu wa kingono hufanyika pia nchini Ujerumani na Denmark kwa hiari, na nchini Poland kama lazima.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.