Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mimi ni sehemu yako, kisogo chako naiga,
Kwa miaka na mikaka, umenielekezani,
Magumu kwangu ondoa, hakuna kama ninangu,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani!
Tumboni ulinibeba, kwa mwiezi tisa yote,
Sana ulichoka tiki, bado ulikakamaa,
Mikononi kanibeba, nikawa kama mchicha,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani!
Usafi ulinifunza, kwa kuniosha kuchao,
Usafi Mungu apenda, mama kumbe ulijua,
Kuvaa ‘linizoesha, sasa kontenti ninayo,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani!
Mienendo bulibuli, ulinipa ninaangu,
Kwenye kijiji nafaa, mimi mui mwema kwao,
Mimi ni mfano mwema, mbele ya walo ja sufi,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani!
Udongo wautifua, bidii yako ni ngome,
Kila siku twala vyema, kwa miko yako ya chuma,
Daima nitakuhifadhi, kama hirizi moyoni,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani.
Kalamu imenigoma, kichongeo kimekwisha,
Mama ni zawadi kwetu, mwombezi wetu mkuu,
Huruma zake tandawa, hututakiya memaa,
Na hakuna mama mwema, kama wewe duniani!
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.