Matukio katika picha Spurs ikitwaa Europa ligi kwa kuichapa Man Utd

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

s

Tottenham wamemaliza ukame wao wa miaka 17 bila taji baada ya bao la Brennan Johnson katika kipindi cha kwanza kutosha kuwachapa Manchester United kwenye fainali ya Europa Ligi.

Ushindi huo unamaanisha kuwa kocha mkuu anayekabiliwa na shinikizo la kufukuzwa, Ange Postecoglou, ametimiza ahadi ya kuleta taji katika msimu wake wa pili Spurs.

s
Maelezo ya picha,Ange Postecoglou

Postecoglou, ambaye alisema “hatawahi kuwa kichekesho” katika hotuba yake kabla ya mechi, alileta tabasamu na furaha isiyo na mipaka kwa mashabiki 15,000 rasmi, na wengi wasio rasmi, wa Tottenham kwenye Uwanja wa San Mames jijini Bilbao.

s
Maelezo ya picha,Mbrazil Richarlison akishangilia medali yake ya dhahabu kwa ushindi dhdi ya Spurs
a
Maelezo ya picha,Nahodha wa Spurs, Son akifurahia kubeba kombi
s
Maelezo ya picha,Mashabiki wa Spurs nao walipata nafasi ya kupiga picha karibu na kombe hilo la kwanza walilolisubiri kwa miaka 17
s
Maelezo ya picha,Kocha Amorin wa United alikuwa mnyonge akipita karibu na komne ambalo Spurs walikabidhiwa baadaye. Hatma yake United haifahamiki
s

Ushindi huu huenda usimuokoe Postecoglou kutimuliwa Spurs katika wiki zijazo. Lakini Muaustralia huyo ataondoka kama shujaa baada ya kocha wa tatu pamoja na Bill Nicholson na Keith Burkinshaw kutwaa taji la Uropa akiwa na vigogo hao wa London Kaskazini.

a
Maelezo ya picha,Kwa wachezaji na banch la ufundi la United, kukosa ubingwa ulikuwa msiba mkubwa kwao, wakihitimisha msibu mbaya zaidi kwenye klabu hiyo

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment