Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna wanawake wengi sana ambao wana ndoto kubwa na wana uwezo mkubwa sana ila kikwazo kikubwa ni kukosa kujiamini:
Inawezekana umepitia maisha magumu sana na Baba YAKO alikukataa ulipozaliwa.Hali hiyo imekusababisha MAISHA YAKO yote ujione ni mtu usiyekubalika na Usiye na thamani maishani mwako.Nakukumbusha kuwa thamani yako ni kubwa mno na ndio maana Mungu aliruhusu UZALIWE.Usikubali KUJIONA hauwezi kwa sababu hiyo.
Umepitia MAUMIVU MAKALI sana siku za hivi karibuni.Umeumizwa na mtu wa karibu sana na imekufanya uwe na usiku wa Vilio mara kwa mara.Kumbuka unayo nafasi ya kufungua ukurasa mpya.Hata kama umepitia jambo gumu kiasi gani,bado unayo fursa ya kufurahia MAISHA tena.Wakati mwingine inabidi ukubali kusamehe,kusahau na kuachilia yaliyopita ili UANZE UKURASA MPYA.
Kuna experience mbaya sana uliipitia kwenye MAISHA YAKO huko nyuma:Uliteswa ama kunyanyasika kijinsia,imeendelea kukutesa hadi leo.Kumbuka kuwa ukitupa DHAHABU kwenye zizi la NG’OMBE wataikanyaga na kuidharau kwa sababu hawajui thamani yake ingawa HAIMAANISHI haina thamani.Wengi waliokutendea mabaya kuna siku watajua walikuwa wanacheza na DHAHABU.
Mapito mengine ni kwa ajili ya kukusaidia kujenga misuli ya MAISHA na kukuandaa uwe Msaada kwa wengine,take it positive.
Unaishi na mtu ambaye kila wakati anakuambia “HAUWEZI”,”HAUTAFIKA MBALI” nk..Isikuvunje moyo.WANAUME wengi tumekulia katika mazingira ya kuaminishwa kuwa wanawake Hawawezi na itachukua Muda kubadilisha mtazamo huo.Hata hivyo wako ambao hujisikia vibaya kuona MWANAMKE anafanikiwa katika kile yeye alichoshindwa.Njia nzuri ya kupambana na hili sio kubishana nao bali ni KUFANYA KWA JUHUDI ILI UPATE MATOKEO.Wanaweza kutoamini Ndoto YAKO bali hawawezi kukataa MATOKEO YAKO. Je,kuna Mwanamke yoyote ukipenda kushare naye ujumbe huu???. Nawatakia wanawake wote wiki ya USHINDI.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.