Mashambulizi ya anga ya Israel yaua watu 40 Gaza – Hospitali

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Zaidi ya watu 40 wameuawa katika mashambulizi ya hivi punde ya Israel katika Ukanda wa Gaza, kulingana na vyanzo vya hospitali.

Kuna ripoti kwamba takriban miili 36 ilipelekwa katika hospitali za kusini, ambazo zilishuhudia mashambulizi makali ya Israel usiku kucha.

Israeli imeongeza mashambulizi yake huko Gaza huku Rais Donald Trump akiendelea na ziara yake eneo la mashariki ya kati katika juhudi za kusitisha mapigano na kufufa mpango wa kuachiliwa kwa mateka.

Zaidi ya watu 52,000 wameuawa na mashambulizi ya Israel, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, na wale ambao wamenusurika wako katika hali mbaya.

Tangu katikati ya mwezi Machi, Israel imezuia chakula cha msaada, dawa na misaada mingine kuingia Gaza.

Kumekuwa na shutuma za kimataifa kuhusu kizuizi hicho, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Umoja wa Mataifa, ambayo imesema kwamba wakazi wa Gaza wapatao milioni 2.1 wako katika “hatari kubwa” ya njaa na wanakabiliwa na “kiwango kikubwa cha uhaba wa chakula”.

Mashirika ya misaada yameambia BBC kwamba watu wana njaa, wanaugua kutokana na maji machafu, na kwamba wanaugua magonjwa yanayotibika.

Israel haiwaruhusu waandishi wa habari wa kimataifa kuingia Gaza, kwa hivyo tunategemea ujumbe, maelezo ya sauti na picha zinazotumwa kwetu na Wagaza moja kwa moja.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment