Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) wanaonekana kuanza awamu mpya ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan baada ya kufurushwa kutoka mji mkuu, katika hatua ambayo baadhi ya wataalam wameitaja kuwa “mkakati wa kufikia utawala haraka”.
Wiki chache tu baada ya jeshi kusherehekea kutwaa tena mji wa Khartoum, adui wake Rapid Support Forces (RSF) wameanzisha mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika Bandari ya Sudan mashariki mwa nchi hiyo.
Mashambulizi hayo yamesababisha hali ya kukatika kwa umeme kuwa mbaya zaidi, huku wakaazi wa jiji hilo wakikumbwa na uhaba wa maji.
“Ni hali ya kukatika kwa umeme katika eneo hili ambayo hatujawahi kushuhudia,” alisema Alan Boswell, mtaalam wa Pembe ya Afrika wa Kundi la Kimataifa la Migogoro.
Msururu wa mashambulizi kwenye mji mkuu na kitovu cha shughuli za kibinadamu kunaashiria kwamba RSF imedhamiria na inaweza kuendelea na vita licha ya hasara kubwa za kimaeneo.
Na imeonyesha kuongezeka kwa vita vya droni barani Afrika.
Ndege zisizo na rubani zimechangia kuongezeka kwa mzozo huo, ambao umeingia mwaka wake wa tatu.
Vita hivyo vilianza kama vita vya kuwania madaraka kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na RSF na vimevutia makundi mengine yenye silaha ya Sudan na waungaji mkono wa kigeni, na kuitumbukiza nchi hiyo katika kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.
Katika miezi ya hivi karibuni RSF wameongeza mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu muhimu ya kiraia katika maeneo yanayodhibitiwa na jeshi, kama vile mabwawa na vituo vya umeme.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.