Rais wa Afrika Kusini kukutana na Trump wiki ijayo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa atasafiri kwenda Marekani kwa ziara ya kikazi wiki ijayo na atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump Mei 21, ofisi ya Ramaphosa ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano.

“Rais Ramaphosa atakutana na Rais Donald Trump katika Ikulu ya Marekani huko Washington DC kujadili masuala ya maslahi ya pande mbili, kikanda na kimataifa,” ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema.

“Ziara ya rais nchini Marekani inatoa fursa ya uwepo wa uhusiano mpya wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili,” iliongeza taarifa hiyo.

Uhusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani umedorora sana tangu Trump arejee Ikulu ya Marekani mnamo mwezi Januari.

Trump amekata misaada yote ya kifedha ya Marekani kwa Afrika Kusini, akitaja kutoridhishwa kwa sera yake ya mageuzi ya ardhi na kesi yake ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya mshirika wa Marekani, Israel.

Wiki hii utawala wa Trump ulikaribisha wazungu 49 wa Afrika Kusini ambao umewapa hadhi ya ukimbizi, baada ya kuwachukulia kuwa wahanga wa ubaguzi wa rangi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment