Kuna tabia ukiwa nazo zitakufanya upoteze hela nyingi sana………

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila siku kuna watu wanajiuliza mbina mimi nikipata pesa hazikai.

Ukipata pesa kidogo zinapotea.

kuna watu wengine wanaaami ni chumaulete…

…kumbe ni tabia zao mwenyewe.

1. Kununua Vitu Bila Mpangilio

Kunawatu hawawezi kukaa na hela…

…wakipata hela wanakuwa wananua vitu bila mpangilio.

Na tabia hii inapoteza pesa nyingi sana…

…na ni muhimu kuamua unatumia pesa gani kwenye jambo gani.

2. Kutumia Pesa Ambayo Haujaipata.

Kuna watu wamekuwa wakitumia pesa ambayo hawajaipata.

Usitumie pesa ambayo siyo halisi.

Yani haujaipata hela unafanya matumizi.

Unakuta mtu anaenda dukani anachukua nguo…

…akiamini kuna hela itaingia.

Na tabia hii imesababisha watu wajikute kwenye madeni…

…na kugombana na watu kwa sababu wanaonekana ni waongo kwa kutumia pesa ambayo hawana.

3. Kutumia Zaidi Ya Wanavyoingiza .

Watu wengi wamekuwa wakitumia pesa zaidi ya wanavyoingiza.

Unakuta mtu kipato chake ni kidogo…

..ila anataka kununua vitu vya gharama kuzidi kipato chake.

Ukitumia pesa nyingi zaidi ya unavyoingiza utaishia kuwa masikini.

4. Kujaribu Kukopa Zaidi Na Zaidi Mpaka Madeni Yanakuzidia.

Kuna watu wanamadeni mengi sehemu mbalimbali.

Na kibaya zaidi ni kwamba watu wengi wanakopa kwa matumizi ya kawaida…

…siyo ya kuingiza faida au ya vitu ambavyo havizalishi.

Tabia hizi ni tabia ambazo ukiwanazo haijalishi una maarifa kiasi gani…

…utaishia kuingia kwenye matatizo makubwa.

Natumai makala hii imekusaidia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment