Familia za waathiriwa wa ajali ya ndege zawasilisha malalamiko dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jeju Air

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Baadhi ya familia za waliofariki katika ajali ya ndege ya Jeju Air mwezi Disemba mwaka jana wamewasilisha malalamishi ya uhalifu dhidi ya watu 15, akiwemo waziri wa uchukuzi wa Korea Kusini na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa shirika hilo la ndege kwa uzembe wa kikazi.

Ndugu za watu 72 walioaga dunia wanataka uchunguzi wa kina zaidi ufanyike kuhusu ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 179 kati ya 181 waliokuwa ndani ya ndege hiyo na kuifanya kuwa ajali mbaya zaidi ya ndege nchini Korea Kusini.

Ajali hiyo “haikuwa ya kawaida tu”, wanadai, lakini “janga kubwa la raia lililosababishwa na usimamizi mbaya wa hatari zinazoweza kuzuilika”.

Takriban miezi mitano sasa, mamlaka bado inachunguza kile ambacho huenda kilisababisha ndege hiyo kuanguka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan na kisha kuwaka moto.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment