Zelensky aahidi ‘kufanya kila kinachowezekana’ kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Putin

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema atasafiri hadi mji mkuu wa Uturuki Ankara kukutana na rais Recep Tayyip Erdogan na atapatikana kwa mazungumzo ya moja kwa moja na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mjini Istanbul siku ya Alhamisi.

“Tutafanya kila kinachowezekana’ kuhakikisha kuwa mkutano huu unafanyika,” aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano uliopangwa kwa haraka huko Kyiv.

Urusi bado haijasema ni nani atakayesafiri kwa ndege hadi Istanbul, ila tu kwamba ingetangazwa “mara tu [Putin] atakapoona inafaa”. Putin na Zelensky wenyewe hawajakutana tangu Desemba 2019.

Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili mara ya mwisho yalifanyika Istanbul, Machi 2022, katika wiki za mwanzo za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Hapo awali Putin alikuwa ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya moja kwa moja huko Uturuki “bila masharti ya awali”, kabla ya Zelensky kutangaza kwamba angeenda yeye binafsi na kutarajia rais wa Urusi pia kusafiri.

Marekani pia inatarajiwa kutuma ujumbe wa ngazi ya juu.

Urusi tayari imeonya kwamba kutoa shinikizo kwa nchi yake “hakuna maana” na haikutoa kauli yake ya mwisho.

Badala yake, imetaka kuangazia suluhu la muda mrefu ambalo linashughulikia kile Urusi inachokiona kama “sababu kuu” za vita – masharti magumu yaliyotangazwa kabla ya uvamizi wa 2022 na kukataliwa mara kwa mara na Ukraine.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment