Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Donald Trump anasema kumekuwa na “marekebisho” katika uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na China kufuatia siku ya kwanza ya mazungumzo kati ya maafisa wa Marekani na China nchini Uswizi.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, rais wa Marekani alielezea mazungumzo hayo kuwa “mazuri sana” na kusema mabadiliko “yamejadiliwa kwa njia ya kirafiki, lakini yenye kujenga”.
Vita vya kibiashara vinavyoongezeka kati ya Washington na Beijing vimeshuhudia rais wa Marekani akipiga bidhaa za China zinazoingia Marekani kwa ushuru wa 145%.
China ililipiza kisasi kwa ushuru wa 125% kwa baadhi ya bidhaa za Marekani.
Kufuatia miezi kadhaa ya piga nikupige, nchi hizo mbili zinakutana huko Geneva wikendi hii kwa mara ya kwanza tangu Trump aipige China kwa ushuru mwanzoni mwa mwaka.
Taarifa chache zaidi kwenye chapisho la jukwaa la kijamii la Truth ni kuwa mazungumzo yanatarajiwa kuendelea Jumapili na yanafanyika kati ya makamu mkuu wa China He Lifeng na Waziri wa Hazina wa Marekani Scott Bessent.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.