Biblia Takatifu. Kutoka 12:1-3
[1]BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,
[2]Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.
[3]Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
Iwe kama wakati wa Musa kwa damu ya mwana kondoo juu ya miimo ya mlango malaika aliwalinda
Damu ya Masihi ukufunike ndani yako,umefanywa kuwa hekaru la Bwana na roho ya Mungu ikae ndani yako
Biblia Takatifu.

Sefania 3:10-12
[10]Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya Kushi, waniombao dua, yaani, binti za watu wangu waliotawanyika, wataleta matoleo yangu.
[11]Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
[12]Lakini nitasaza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.
Popote ulipo uwe na nguvu yake Bwana damu ya Yesu iwe kwa kila jambo utaishi na utashinda wewe ni mteule auta angamia
YAKOBO 5;7 7 K
Hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.