Pakistan imetoa mamlaka kwa jeshi kuchagua wakati na jinsi ya kujibu mashambulizi ipasavyo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu wakikagua msikiti ulioharibiwa kufuatia shambulizi la India huko Muzaffarabad huko Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan.

Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan ameita shambulizi la India kuwa “uchokozi wa aibu na woga”, ambao alisema unalenga “raia wenye amani, wakiwemo wanawake na watoto”.

Akiongea na kipindi cha Newshour cha BBC World Service, Ahsan Iqbal anasema madai ya India kwamba ilikuwa inalenga kile ilichokiita “maeneo ya miundombinu ya kigaidi” nchini Pakistan na Kashmir inayotawaliwa na Pakistan ni “uongo mkubwa” ambapo ilikuwa “inajaribu kupotosha ulimwengu”.

“Majeruhi ni akina nani? Mtoto wa miaka saba anawezaje kuwa gaidi? Inakuwaje msichana wa miaka mitano awe gaidi? Inakuwaje mama wa nyumbani, mwanamke awe gaidi?” anauliza.

Akizungumzia hatua ya Pakistan, alisema kuwa serikali ya Pakistani imewapa wanajeshi “mamlaka ya kuchagua wakati na jinsi tunaweza kujibu ipasavyo”.

Wanajeshi wa Pakistan wametangaza idadi ya vifo kufuatia mashambulizi ya India ya usiku kucha.

Msemaji wa jeshi anasema watu 31 wameuawa na 57 kujeruhiwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment