Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

India imetoa taarifa hivi punde ikisema kwamba imekabiliana na majaribio ya Pakistan katika usiku wa Jumatano na Alhamisi “uliolenga maeneo kadhaa ya kijeshi” kaskazini na magharibi mwa India kwa kutumia “droni na makombora”.
Taarifa ya India inaongeza kuwa ililenga Rada za Ulinzi wa Anga na mifumo katika “maeneo kadhaa” nchini Pakistan.
“Imefahamika kuwa mfumo wa Ulinzi wa Anga huko Lahore umeshambuliwa,” ilisema.
Taarifa hiyo haitoi maelezo zaidi kuhusu jinsi India ilivyolenga mifumo hiyo.
Pakistan imedai ilidungua ndege 25 zisizo na rubani za India tangu jana usiku.
Na India inadai kwamba Pakistan ilituma “droni na makombora” katika maeneo kadhaa nchini India.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.