Rihanna afichua kuwa ana ujauzito wa mtoto wa tatu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rihana

Mwimbaji Rihanna amethibitisha kuwa anatarajia mtoto wake wa tatu wakati akihudhuria usiku mkubwa wa mwaka wa mitindo, Met Gala huko New York.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alikumbatia tumbo lake na kutabasamu mbele ya kamera akiwa kwenye zulia jekundu.

Rihanna, ambaye jina lake halisi ni Robyn Fenty, na mpenzi wake, rapa A$AP Rocky, tayari wana watoto wawili wa kiume.

A$AP Rocky, anayejulikana pia kama Rakim Mayers, aliwashukuru wanahabari ambao walitoa pongezi zao kwenye zulia jekundu. “Ni wakati wa kuwaonesha tu watu kile tulichokuwa tunakipika,” alisema.

A$AP Rocky, mwenyekiti mwenza wa hafla hiyo, alithibitisha habari za ujauzito wa wanandoa hao kwenye zulia jekundu. “Asante, asante, asante,” rapper huyo alisema. “Nina furaha kila mtu ana furaha kwa ajili yetu kwa sababu hakika tuna furaha”, aliongeza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment