Funguo 5 Unazoweza Kutumia Ili Kuharakisha Maono Yako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Jitambue Wewe Ni Nani Mbele Za Mungu

ii. Wekeza Katika Maarifa

iii. Kuwa Mtatuzi Wa Matatizo

iv. Uwe Mwenye Bidii

v. Uwe Mtu Wa Kuchukua Hatua

Katiba Makala Hii Tutazungumzia Funguo Ya Tatu

– Kuwa Mtatuzi Wa Matatizo

Dunia inatafuta watatua matatizo.

Watu ambao wanafanya haraka kutatua matatizo ya wengine…

…ndio ambao pia wanafanikiwa kwa haraka katika maono yao.

Kama unataka kutimiza maono yako kwa kasi…

…badala ya kujiunga na watu wanaolalamika kila siku.

Jiunge na watu ambao wanatafuta suluhisho la matatizo mbalimbali yanayowakabili.

Bila kujali kabila, jinsia au rangi yako, ukiwa mtu…

…unayetatua matatizo kwenye jamii lazima utakuwa mtu muhimu.

Hata kama watu wanajifanya hawakufahamu au kukutambua…

…ukianza tu kutatua matatizo, utaanza kukumbukwa na kupewa heshima yako.

Yusufu kwa sababu alikuwa mtu anayejikita katika kutatua matatizo…

…ingawa alisahaulika kwa miaka miwili akiwa gerezani, ila alikuja kukumbukwa (Mwanzo 41:1).

Watu wanaojikita katika kutatua matatizo lazima watakumbukwa tu.

Daudi alifanikiwa kuwa mfalme kwa sababu alitatua tatizo.

Ingawa wakati baba yake ameambiwa awaite watoto kwa ajili ya kuchagua mfalme, Daudi alisahaulika kabisa.

Ila baada ya kutatua tatizo lililokuwa linakabili Taifa, maono aliyopewa na Mungu ya kuwa kiongozi yakatimia.

Kumbuka unapokimbia matatizo, hapo unakimbia fursa ya kutimiza maono yako.

Matatizo ni fursa kwa watu ambao wana maono.

Kadiri unavyotatua matatizo ya watu wengi ndivyo utakavyofanikiwa haraka.

Na kadiri unavyotatua matatizo makubwa ndivyo utakavyofanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Kila unayemuona amefanikiwa, kuna matatizo ambayo anatatua.

Ni kweli unamwomba Mungu akusaidie kutimiza maono yako.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment