Polisi wazingira nyumbani kwa Viongozi wa Chadema,

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.
Maelezo ya picha,Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu

Polisi wenye silaha wamezingira nyumbani kwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, chadema Tundu lisu pamoja na nyumbani kwa makamu mwenyekiti John Heche.

Hata hivyo Polisi hawajathibitisha kuzingira nyumba za viongozi hao wa Upinzani

Kupitia mtandao wa kijamii Heche ameandika “nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa kumi alfajiri ya leo, askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia” .

Haya yanajiri wakati mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo inasikiliza upande wa Jamhuri(Mleta mashtaka) juu ya hoja za mawakili wa Lisu waliopinga kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya mtandao .

Polisi walisisitizia wanachama wa Chadema kutokwenda mahakamani wakisema ni kwa lengo la kuimarisha amani huku Makamu Mwenyekiti wa Chadema John heche akiwahamasisha wanachama wao kwenda kwani ni haki yao ya kikatiba.

Nje ya Mahakama ulinzi umeimarishwa huku Wanachama wa Chadema na waandishi wa habari wakiwa wamezuiwa kuingia mahakamani.

Tundu Lisu anakabiliwa na mashtaka mawili ya uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii na uhaini ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa may 6.

Alikamatwa tangu April, 10, 2025 na yuko ndani kwa kesi ya uhaini ambayo haina dhamana.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment