Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wafanyakazi wa misaada nchini Sudan wameripoti kuwa watoto ni miongoni mwa wanaofariki kwa kiu na njaa, baada ya kulazimika kukimbia kambi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani nchini humo.
Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa shambulio la hivi karibuni lililofanywa na wanamgambo wa RSF imesababisha wimbi la uhamishaji wa watu ambalo halijawahi kushuhudiwa katika historia ya eneo hilo.
Kati ya watu waliokuwa wamekimbilia usalama katika kambi ya Zamzam, iliyoko katika eneo la Darfur, inakadiriwa kuwa walikuwepo kati ya nusu milioni hadi 700,000.
Hata hivyo, wiki mbili zilizopita, sehemu kubwa ya kambi hiyo iliharibiwa kwa moto, na mashambulizi hayo kusababisha vifo vya raia pamoja na wafanyakazi wa misaada.
Wengi wa waliolazimika kukimbia wamepoteza maisha kutokana na njaa na kiu, huku joto kali likizidi nyuzi joto 40.
Baadhi yao waliweza kuwasili katika mji wa Tawila, ambako misaada ya kibinadamu inaendelea kutolewa japo ni wa kiwango cha chini.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.