Rais wa Ghana akosolewa kwa kumsimamisha kazi Jaji Mkuu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jaji Gertrude Torkornoo

Wabunge wa upinzani nchini Ghana wamelaani vikali hatua ya kusimamishwa kazi kwa Jaji Mkuu wa nchi hiyo, wakimtuhumu Rais John Mahama kwa jaribio la kupenyeza ushawishi wa kisiasa mahakamani kwa kuwateua majaji wenye mwelekeo wa kuiunga mkono serikali.

Jaji Mkuu Gertrude Torkornoo aliondolewa madarakani siku ya Jumatano, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa Jaji Mkuu kusimamishwa kazi.

Uamuzi huo ulitolewa kufuatia kuwasilishwa kwa mapendekezo matatu ya siri yaliyoibua tuhuma dhidi ya Bi. Torkornoo, yakitaka aondolewe kabisa katika wadhifa huo.

Bi. Torkornoo ni Jaji Mkuu wa tatu mwanamke katika historia ya Ghana, na aliteuliwa mwaka 2023 na Rais Nana Akufo-Addo.

Waziri wa zamani wa sheria, Bw. Godfred Yeboah Dame, aliieleza BBC kuwa hatua ya kumsimamisha kazi Bi. Torkornoo ni “mchakato usio na msingi… shambulio kubwa zaidi dhidi ya mhimili wa mahakama katika historia ya taifa.”

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Bi. Torkornoo aliweza kunusurika jaribio la kuondolewa madarakani mapema mwaka huu, baada ya Rais Akufo-Addo kueleza kuwa ombi hilo lilikuwa na mapungufu kadhaa ya kisheria.

Kamati maalum ya watu watano imeundwa ili kuchunguza kwa kina tuhuma zinazomkabili Bi. Torkornoo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment