Maelfu ya watu waendelea kumuaga Papa Francis

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

x

Maelfu ya watu wanaendelea kupanga foleni katika kanisa kuu la Mtakatifu Petro wakisubiri kutoa heshima zao kwa Papa Francis. Anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa Vatican watu takriban 90,000 wamempa heshima za mwisho Papa Francis.

Mkuu huyo wa Kanisa Katoliki alifariki kutokana na maradhi ya kiharusi siku ya Jumatatu, akiwa na umri wa miaka 88, chini ya saa 24 baada ya kuongoza hotuba ya Pasaka.

Afya yake ilizorota baada ya kukabiliwa na homa kali ya mapafu hivi karibuni.

Viongozi kadhaa duniani wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer, Rais wa Marekani Donald Trump, Mwana wa Mfalme wa Wales, na Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil.

Maelfu ya waombolezaji tayari wamemiminika katika jiji la Vatican, wakiwa wamebeba maua, misalaba na mishumaa na kukariri sala.

Mazishi yataanza saa 10:00 katika uwanja ulio mbele ya Basilica ya St Peter. Mababu, makadinali, maaskofu wakuu, maaskofu, na makasisi kutoka kote ulimwenguni watashiriki.

Mkuu wa Chuo cha Makardinali, Kadinali Giovanni Battista Re, ndiye atakayeongoza ibada hiyo.

Kardinali Battista Re atatoa sala ya kuhitimisha ambapo Papa atakabidhiwa rasmi kwa Mungu na mwili wa Papa utahamishiwa St Mary Meja kwa maziko.

Kipindi cha maombolezo cha siku tisa, kinachojulikana kama Novemdiales, kisha kitaanza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment