ACHA HOFU USIWE MTU WAKUPENDA TAARIFA MBAYA JIPE MATUMAINI KTK MUNGU WAKO.
Mpendwa lazima ujikinge lakini baki katika Imani juu ya Mungu
Dunia itatengeneza vitisho vingi kuambatanisha na hili.

“Lakini kama Mungu wetu aishivyo hatutaogopa chochote mbele yetu.”
Zaburi:27.1
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Daudi aliimba wimbo huu akiwa amekabiliwa na maadui wa ndani na nje Basi jitie nguvu kwa Bwana ktk hili.
TUMTAZAME YESU KRISTO PEKEE
MAANA KAMA ULE MWISHO BADO HATAONDOKA HATA MMOJA KABLA YA WAKATI ULIOKUSUDIWA NA MUNGU. Tuone kusudi la Ufalme wake Mungu ktk kipindi hiki kigumu Cha watu na mataifa kukimbizana na CORONER wajuaje MUNGUanataka turejee kwake? Ikiwa nitaleta tauni na kukosa mvua nk IKIWA WATU WALIOITWA KWA JINA LANGU WATAJINYENYEKESHA NA KUOMBA NA KUNITAFUTA USO NA KUZIACHA NJIA ZAO MBAYA BASI NITASIKIA TOKA MBINGUNI NA KUWASAMEHE DHAMBI YAO NA KUIPONYA NCHI YAO 2 Nyak 7:13-14
USIRUHUSU HOFU IKUUE MWAMINI MUNGU
Zaburi:91.3
Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo ( tauni Ni ugonjwa unaoambukiza toka mtu na mtu au myama na mtu).
Zaburi:91.4
Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao ndani yako mpendwa ona kufunikwa na Bwana wakati watu wanatafuta Nini kiwafunike jifunike kwa Damu ya Yesu Kristo Bwana .
Zaburi:91.5
Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana Kama nilivyosema mwanzo ukiogopa ufungulia wa hofu Goliath aliwatisha wanaisrael wakiwa na mfalme wao lakini Daudi aliondoa hofu Wala hakuogopa ndo akaweza kumuua Goliath, ndugu yangu mpendwa jiambiea coroner lazima Ife na kufariki ndani yangu na nchini amen
Zaburi:91.6
Wala tauni ( coroner) ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri mpendwa sema na mipaka ya Nchi yetu, mikoa,wilaya,tarafa kata,vijiji,mitaa na nyumba inasikia ili tauni isivuke.
Zaburi:91.7
Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

MUNGU NI MWEMA KWA VIUMBE WAKE SHALOM

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.