Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani mashambulizi ya Urusi yaliyotokea Ukraine.
Ujumbe wake kwenye akaunti ya mtandao wa kijami wa Truth Social, ameandika: “Sijafurahishwa na mashambulizi ya Urusi huko KYIV. Hakuna haja ya kufanya hivyo, na ni wakati mbaya sana. Vladimir, Acha! Wanajeshi 5000 wanakufa kwa wiki. Makubaliano ya amani YAFIKIWE!”
Urusi inadai mashambulizi nchini Ukraine yalilenga miundombinu ya kijeshi
Wizara ya ulinzi ya Urusi inadai kuwa mashambulizi hayo yalilenga “usafiri wa anga, roketi na anga, makampuni ya ujenzi wa mashine na viwanda vya vifaru nchini Ukraine, makampuni yanayozalisha mafuta ya roketi na baruti”.
“Maeneo lengwa ya shambulizi hilo yamefikiwa. Yote yameshambuliwa,” wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa.
Ujumbe wa Trump umejitokeza saa chache baada ya Trump kumkosoa rais wa Ukraine kwenye jukwaa hilo hilo.
“Yeye [Zelensky] anaweza kuwa na amani au, anaweza kupigana kwa miaka mingine mitatu kabla ya kupoteza nchi nzima,” Trump aliandika Jumatano, akiongeza kuwa Zelensky ndiye “asiye na chaguo la kumwezesha kufanikiwa”.
Ujumbe wa Trump kwa Putin ni nadra sana kulaani mashambulizi ya kila siku ya Urusi dhidi ya Ukraine – na ishara ya kufadhaika kwake.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.