Urusi yaishambulia Kyiv kwa kombora na droni – Meya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

dc
Maelezo ya picha,Waokoaji huko Kyiv wanatafuta katika mabaki ya jengo la makazi lililoharibiwa na shambulizi la usiku la Urusi.

Takriban watu tisa wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, katika shambulio la usiku la kombora la Urusi na ndege zisizo na rubani kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, amesema afisa wa eneo hilo.

Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko amesema mabaki ya droni iliyoanguaka imesababisha moto, na kuna hofu kwamba watu kadhaa wamenasa chini ya vifusi vya jengo la makazi lililoharibiwa.

Milipuko pia iliripotiwa katika mji wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv. Takriban watu wawili walijeruhiwa huko, amesema Meya.

Haya yanajiri saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kumshutumu Volodymyr Zelensky kwa kuharibu mazungumzo ya amani, baada ya rais wa Ukraine kukataa kutambua udhibiti wa Urusi wa eneo la Crimea.

Ukraine imerudia kusema haitaiacha Crimea, peninsula ya kusini iliyonyakuliwa kinyume cha sheria na Urusi mwaka 2014.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alifanya uvamizi dhidi ya Ukraine mwaka 2022, na Moscow kwa sasa inadhibiti karibu 20% ya ardhi ya Ukraine.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment