Trump amkosoa Zelensky kwa kukataa Urusi kudhibiti Crimea

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kwa kuharibu mazungumzo ya amani, baada ya rais wa Ukraine kusema Kyiv haitatambua udhibiti wa Urusi kwa eneo la Crimea.

Kupitia Mtandao wake wa Kijamii wa Truth Social, Trump amedai makubaliano ya kumaliza vita yalikuwa “karibu sana,” lakini kukataa kwa Zelensky kukubali masharti ya Marekani “kutarefusha” mzozo.

Ukraine kwa muda mrefu imesema haitaiacha Crimea, rasi ya kusini iliyonyakuliwa kinyume cha sheria na Urusi tangu mwaka 2014 kuwa sehemu ya Urusi.

Hapo awali Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance alisema makubaliano ya amani yatamaanisha Ukraine na Urusi “zote zitalazimika kuacha baadhi ya maeneo wanayomiliki kwa sasa.”

Marekani bado haijatoa maelezo hadharani kuhusu makubaliano gani ya kijiografia yangepaswa kufanyika.

Alipoulizwa na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kuhusu iwapo utawala huo unatazamia kutambua mamlaka ya Urusi juu ya Crimea, Trump amesema anataka tu kuona vita hivyo vikimalizika.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment