Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, John Heche na viongozi wengine wa chama hicho, wameachiliwa huru na jeshi la polisi saa chache baada ya kukamatwa wakati wakijiandaa kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam.
Heche ameiambia BBC, “Polisi hawakuwa na sababu ya kweli ya kutukamata. Baada ya saa za kukamatwa, sasa tuko nje bila masharti yoyote. Sisi chama cha Chadema tumedhamiria na tutazungumza na umma kesho (Jumatano).”
Heche alikamatwa na Jeshi la Polisi katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ambapo kwa kwa mujibu wa taarifa kutoka CHADEMA, Heche alikwenda kuongoza mkutano wa hadhara ambao tayari ulitangazwa na taarifa kuwasilishwa kwa Polisi siku kadhaa zilizopita.
Hata hivyo, Polisi walileta barua saa chache kabla ya mkutano kuanza, wakipinga kufanyika kwake kwa madai kuwa eneo la mkutano Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni lina shughuli nyingi za biashara na mkutano huo ungeathiri shughuli hizo.
Licha ya zuio hilo, Heche alifika eneo la mkutano, ambapo Polisi walimkamata na kuondoka naye.
Kukamatwa kwa Heche na kuachiwa kunakuja wiki chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhaini, mashtaka ambayo hayana dhamana.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.