Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Sikua ya Jumanne Rais Donald Trump amesema ikiwa China haitakubali makubaliano ya biashara, Marekani itaweka masharti.
Trump pia amewaambia waandishi wa habari, atakuwa mwema katika mazungumzo na Beijing na ushuru wa bidhaa kutoka nchi hiyo utapungua kwa kiasi kikubwa ikiwa kutakuwa na makubaliano, lakini sio kuondoa ushuru moja kwa moja.
Matamshi ya Trump yalikuwa kujibu maoni ya siku ya Jumanne ya katibu wa hazina Scott Bessent, ambaye alisema ushuru wa juu sio endelevu na anatarajia vita vya Biashara vitapungua kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.
Trump ameweka ushuru wa 145% kwa bidhaa China, nayo imeweka ushuru wa 125% kwa bidhaa kutoka Marekani.
Trump ameweka ushuru kwa nchi kadhaa, na kusababisha soko la hisa kushuka na viwango vya riba kuongezeka katika deni la Marekani huku wawekezaji wakihofia kuzorota kwa uchumi na mfumuko wa bei.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.