Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwili wa Papa Francis umeingizwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro baada ya kupitishwa katika uwanja wa St Peter’s Square kutokea katika makazi yake.
Kutakuwa na ibada ya maombi kabla ya umma kuruhusiwa kuingia ili kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Papa kuanzia leo.
Papa Francis, aliyekuwa mkuu wa Kanisa Katoliki, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Mazishi ya Papa yamepangwa kufanyika Jumamosi, Aprili 26, kulingana na Vatican, huku viongozi mbalimbali wa dunia wakitarajiwa kuhudhuria.
Kifo cha Francis siku ya Jumatatu kilikuja baada ya msururu wa matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kugundulika kuwa na nimonia ambayo ilimweka hospitalini kwa zaidi ya mwezi mmoja mapema mwaka huu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.