Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu tisa wameuawa baada ya ndege isiyo na rubani ya Urusi kushambulia basi lililokuwa likisafirisha wafanyikazi nchini Ukraine, maafisa wanasema.
Shambulio hilo lilitokea Jumatano asubuhi katika mji wa kusini wa kati wa Marhanets.
Serhiy Lysak, mkuu wa mkoa wa Dnipropetrovsk, alisema takriban watu 30 walijeruhiwa, akiongeza kuwa “idadi ya waathiriwa inakua kila wakati”.
Shambulio hilo limetokea wakati maafisa kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani na Ukraine wakijiandaa kufanya mazungumzo mjini London kwa lengo la kuafiki usitishaji mapigano katika mzozo huo.
Urusi ilianzisha uvamizi dhidi ya Ukraine mnamo tarehe 24 Februari 2022. Inakadiriwa kuwa mamia ya maelfu ya watu wameuawa au kujeruhiwa kila upande tangu wakati huo.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa ametangaza kusitisha mapigano kwa saa 30 kwa Jumapili ya Pasaka.
Hata hivyo, kila upande ulimtuhumu mwenzake kwa kuvunja mapatano hayo.
Mwezi uliopita, Moscow ilikuja na orodha ndefu ya masharti kukubali usitishaji vita ambao ulikuwa umekubaliwa na Marekani na Ukraine.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.