Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Siku ya Jumatatu, Rais wa Urusi Vladimir Putin alipendekeza mazungumzo baina ya nchi yake na Ukraine, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita.
Naye Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amesisitiza katika hotuba yake ya kila usiku ya video kwamba Ukraine “iko tayari kwa mazungumzo yoyote” kuhusu usitishaji mapigano ambao ungesimamisha mashambulizi kwa raia.
Viongozi hao wawili wanakabiliwa na shinikizo kutoka Marekani, ambayo imetishia kuachana na juhudi zake za kutafuta amani iwapo hakuna maendeleo yatapatikana.
Urusi na Ukraine zimesema ziko tayari kusitisha mapigano zaidi baada ya mpango wa kusitisha vita wakati Pasaka kwa saa 30 uliotangazwa na Moscow mwishoni mwa juma. Kila upande ulimtuhumu mwenzake kukiuka mpango huo.
Ukraine itashiriki katika mazungumzo na Marekani na nchi za Ulaya siku ya Jumatano mjini London, Zelenskiy alisema. Majadiliano hayo ni muendelezo wa mkutano wa Paris wiki iliyopita ambapo Marekani na mataifa ya Ulaya yalijadili njia za kumaliza vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.
Putin, akizungumza na ripota wa runinga ya serikali ya Urusi, alisema mapigano yalianza tena baada ya kusita mapigano wakati wa Pasaka, na kusema Moscow, iko wazi kwa mipango yoyote ya amani na anatarajia utayari kama huo kutoka Kyiv.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.