Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makadinali wa Vatican, wanakutana leo kwa mara ya kwanza kuamua ni lini mwili wa Papa Francis utapelekwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro – na ni lini mazishi yatafanyika.
Kulingana na katiba ya kitume – mazishi hayo yanapaswa kufanyika “kati ya siku ya nne hadi ya sita baada ya kifo.”
Hilo litaifanya tarehe ya mazishi kuwa kati ya Ijumaa 25 Aprili – Siku ya Ukombozi nchini Italia, likizo ya kitaifa – na Jumapili 27 Aprili.
Vyombo vingi vya habari vya Italia vinaripoti kuwa mazishi huenda yakapangwa Jumamosi, huku shirika la habari la kitaifa Ansa likinukuu vyanzo vya Vatican.
Wakati huo huo, Vatican imetoa picha za Papa Francis katika jeneza lake lililo wazi, akiwa amevalia vazi jekundu na kilemba cha papa kichwani na rozari mkononi mwake.
Picha hizo zilichukuliwa katika kanisa la Casa Santa Marta, makazi ya Francis huko Vatican.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.