Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Afisa mkuu wa Palestina anayefahamu mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas ameiambia BBC kwamba wapatanishi wa Qatar na Misri wamependekeza mfumo mpya wa kumaliza vita huko Gaza.
Kulingana na afisa huyo, inatazamia kufikiwa kwa makubaliano ya amani ya kudumu kati ya miaka mitano hadi saba, kuachiliwa kwa mateka wote wa Israel kwa mabadilishano wa wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel, kukomesha rasmi vita, na Israel kujiondoa kabisa Gaza.
Ujumbe mkuu wa Hamas ulipaswa kuwasili Cairo kwa mashauriano.
Makubaliano ya mwisho ya kusitisha vita yalisambaratika mwezi mmoja uliopita wakati Israel ilipoanza tena kulipua Gaza, huku pande zote mbili zikilaumiana kwa kushindwa kuendeleza makubaliano hayo.
Israel haijatoa maoni yoyote kuhusu mpango wa wapatanishi.
Wakati huo huo, Wapalestina 22 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza tangu Jumatatu jioni, afisa wa afya katika wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas aliambia BBC.
Afisa huyo alisema waliuawa katika maeneo ya Khan Younis, Jabalia, Beit Lahia, na mji wa Gaza, na kwamba watu wengine 45 walijeruhiwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.